Hayo yamesemwa na Muhammad Bunyadi Mshauri wa Waziri wa Elimu wa Iran katika masuala ya Qur'ani ambaye amesema katika mahojiano na IQNA kuwa mpango wa kuongeza madrasa za Qur'ani unatokana na maombi ya mikoa yote nchini. Amesema kuwa kufuatia uamuzi wa Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni, Wizara ya Elimu imepewa jukumu la kuendesha shughuli za madrasa za Qur'ani hapa nchini. Amesema katika mwaka mpya wa masomo unaoanza Februari, madrasa elfu 10 za Qur'ani zitafunguliwa nchini Iran.
Ameongeza kuwa madrasa za Iran nje ya nchi pia zitaanza kutoa mafunzo maalumu ya Qur'ani kwa wanafunzi, wazazi na Wairani wote waishio nje ya nchi ambao wana raghba ya kujifunza Qur'ani Tukufu.
Mshauri wa Waziri wa Elimu Iran amesema pia kuna mpango wa kutoa mafunzo ya mbinu mpya za kufundisha Qur'ani kwa waalimu nchini. Amesema waalimu sabini elfu watapata mafunzo maalumu kuhusu mbinu mpya za kufundisha Qur'ani.
Aidha afisa huyo wa Wizara ya Elimu Iran amesema wanaosoma katika madrasa za Qur'ani nchini hawatatozwa karo yoyote. Amesema wanaotaka kutoa mchango kwa madrasa za Qur'ani wanaweza kutuma misaada yao kupitia akaunti ya benki ya wizara ya elimu.
734220