IQNA

Vikao vya masomo ya Qur'ani Tukufu vyaanza Afrika Kusini

11:51 - January 22, 2011
Habari ID: 2068432
Vikao vya mafunzo ya hifdhi ya Qur'ani Tukufu vilianza jana Ijumaa huko katika mji wa Cape Town Afrika Kusini na vitaendelea hadi Jumatatu tarehe 24 mwezi huu wa Januari.
Mahafidh wa Qur'ani kutoka Afrika Kusini na Afrika Mashariki wanashiriki katika vikao hivyo ambavyo vimeandaliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO.
Masomo hayo ya muda mfupi ambayo yameandaliwa katika fremu ya shughuli za Taasisi ya Kimataifa ya Hifdhi ya Qur'ani inayofungamana na Jumuiya ya Kimataifa ya Kiislamu yanatekelezwa kwa msaada wa Uongozi wa Masuala ya Qur'ani na Baraza la Waislamu wa Afrika Kusini. Wawakilishi 22 kutoka nchi 12 za Afrika wanashiriki katika masomo hayo. Vikao hivyo vimeandaliwa kwa ajili ya kuwashukuru na kuwaenzi mahafidh wa Qur'ani Tukufu na vilevile kurahisisha masuala ya kuhifadhi Qur'ani kupitia vikao, uimarishaji na tathmini ya shule za Qur'ani Tukufu.
Kubadilishana uzoefu katika nyanja za masomo ya Qur'ani, kubainishwa mbinu mpya za kuhifadhi Qur'ani, ushirikiano na kujuana zaidi wataalamu wa masuala ya mafunzo ya Qur'ani pamoja na kubadilisha uzoefu wao ni malengo mengine ya kufanyika vikao hivyo. 734243
captcha