Kwa mujibu wa Kapteni Mehdi Meidani Naibu Mkurugenzi wa Chuo cha Darul Qur'an katika Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, mashindano ya Qur'ani ya “Urafiki wa Majeshi ya Iran na Oman” yatafanyika katika Ukumbi wa Kauthar mjini Tehran.
Amesema mahafiidh wa Qur'ani kutoka nchi hizo mbili watashindana na hatimaye washiriki bora wanne watatunukiwa zawadi katika viwango vinne vya kuhifadhi juzuu sita, kumi, kumi na nane na Qur'ani Kamili.
Ameongeza kuwa idadi ya washiriki itakuwa 24, yaani 12 kutoka kila nchi, na kwamba jopo la majaji linajumuisha wataalamu wa Qur'ani kutoka Iran.
Kapteni Meidani amesema sherehe za kufunga mashindano hayo zitahudhuriwa na Karim Mansouri, karii maarufu wa Qur'ani nchini Iran.
734548