IQNA

Wanafunzi kutoka nchi 52 watembea kwa miguu kuelekea Karbala

10:30 - January 24, 2011
Habari ID: 2069081
Zaidi ya wanafunzi 500 wa masomo ya kidini kutoka nchi mbalimbali za Kiarabu, Asia, Ulaya, Marekani na Australia na Afrika wanashiriki katika matembezi marefu ya miguu kuelekea katika mji mtakatifu wa Karbala nchini Iraq ili kushiriki katika maombolezo ya Arbaini ya Imam Hussein (as).
Hujjatul Islam wal Muslimin Sheikh Ridha az-Zubeidi, mmoja wa wakuu wa ofisi ya Ayatullahil Udhma Sayyid Muhammad Said Hakim, mmoja wa mamarja' wanaoishi katika mji mtakatifu wa Najaf amesema kuwa zaidi ya wanafunzi 500 wa masomo ya kidini kutoka katika nchi 52 za dunia wanashiriki katika matembezi hayo kuelekea Karbala.
Amesema wanafunzi hao wanashiriki katika msafara mkubwa wa mamilioni ya waombolezaji wanaotembea kwa miguu kuelekea katika mji huo.
Katika siku ya kukaribia Arbaini ya Imam Hussein hapo siku ya Jumanne, mamilioni ya wapenzi wa Watu wa Nyumba ya Mtume (saw) wanatembea kwa miguu kutoka miji mbalimbali ya Iraq kuelekea mji wa Karbala. 734910
captcha