IQNA

Maombolezo ya Arbaini ya Imam Hussein (as) kufanyika mjini London

13:41 - January 24, 2011
Habari ID: 2069650
Maombolezo ya Arbaini ya Imam Hussein (as) yamepangwa kufanyika tarehe 30 Januari huko London mji mkuu wa Uingereza.
Kwa mujibu wa tovuti ya Jafariya News, maombolezo hayo ambayo yameandaliwa na Taasisi ya Husseini ya Uingereza, yataanza kwa swala ya jamaa ya Adhuhuri.
Hotuba mbalimbali kuhusiana na Imam Hussein (as) na mapambano yake ya Ashura pamoja na ziara ya Arbaini ya Imam huyo mtukufu ni miongoni mwa ratiba zilizopangwa kutekelezwa katika siku hiyo.
Kwa mujibu wa tangazo la taasisi hiyo mifano ya makaburi ya Imam Hussein, Hadhrat Abbas na Ali Asghar (as) yataonyeshwa katika maombolezo hayo. 735318
captcha