Hayo yamesemwa na mhadhiri wa Chuo cha Bosnia na Taasisi ya Mulla Sadra Artan Besrek wakati alipotembelea kituo cha Nour cha Qum nchini Iran na kuongeza kuwa kuwepo mji huo mtakatifu na Kituo cha Uhakiki wa Komputa wa Sayansi za Kiislamu ni fahari kubwa kwa ulimwengu wa Kiislamu.
Akiashiria programu za kumputa zinazozalishwa na kituo hicho amesema kuwa shughuli zote za kituo hiki cha kielimu zina mvuto makhsusi kama ilivyo dini ya Kiislamu.
Artan Besrek amongeza kuwa bidhaa zinazozalishwa katika Kituo cha Uhakiki wa Komputa wa Sayansi za Kiislamu zinawafaidisha si Wairani na Asia pekee bali Waislamu wote zaidi ya bilioni moja kote duniani.
Mhadhiri huyo wa chuo cha Bosnia amesisitiza kuwa Uislamu ni hadiya na zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu SW kwa ajili ya wanadamu na Waislamu wanapasa kufanya jitihada kubwa za kuilinda dini hiyo. 735602