IQNA

Mamilioni washiriki maombolezo ya Arubaini ya Imam Hussein AS

13:41 - January 26, 2011
Habari ID: 2070193
Mamilioni ya Waislamu wamefika katika mji mtakatifu wa Karbala nchini Iraq kwa ajili ya kushiriki kwenye maombolezo ya Arubaini ya mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) Imam Hussein (AS).
Inakadiriwa kuwa watu milioni 10 walishiriki katika maombolezo hayo wakiwemo wafanyaziara Wairaqi na wageni kutoka maeneo mbalimbali duniani. Kilele cha maombolezo hayo kilikuwa Jumanne 20 Safar 1432 Hijria. Usalama uliimarishwa mjini Karbala ambapo maafisa laki moja 20 elfu walilinda doria kwenye mji huo. Jumatatu iliyopita watu wasiopungua 14 waliuawa shahidi na wengine zaidi ya 141 kujeruhiwa katika mashambulizi ya mabomu yaliyowalenga wafanyaziara mjini Karbala.
Mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) Imam Hussein bin Ali bin Abi Twalib (AS) aliuawa shahidi kinyama mwaka 61 Hijria kwa amri ya mtawala dhalimu wa wakati huo Yazid bin Muawiya.
Mtukufu huyo amezikwa katika mji mtakatifu wa Karbala ulioko umbali wa kilomita 110 kusini mwa Baghdad.
736416
captcha