Muhammad Mahmoud, Mkuu wa Idara ya Tablighi na Muongozo wa Kiislamu ya Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Qatar amesema kuwa mashindano ya 18 ya kimataifa ya hifdhi na tajwidi ya Qur'ani Tukufu yatafanyika nchini humo hivi karibuni.
Amesema usajili wa majina ya washiriki wa mashindano hayo yaliyopewa jina la Sheikh Jassim bin Muhammad Aal Thani, usajili ambao utakuwa ukifanyika kila siku, ulinza jana na umepangwa kuendelea hadi tarehe 5 Februari. Ameongeza kuwa mashindano hayo ambayo yatafanyika katika makundi mawili ya hifdhi na tajwidi ya Qur'ani Tukufu yatafanyika katika hatua saba za hifdhi ya Qur'ani nzima pamoja na usomaji wa tajwidi na tartili, hifdhi ya juzuu 25 tajwidi na tartili, hifdhi ya juzuu 20 tajwidi na tartili, hifdhi ya juzuu 15 na usomaji wa tartili na tajwidi, hifdhi ya juzuu 10 na usomaji wa tartili na tajwidi, hifdhi ya juzuu 5 na tartili na tajiwidi na hatimaye hifdhi ya juzuu moja kati ya juzuu tano za mwisho za Qur'ani Tukufu.
Hatua hii ya mwisho itawahusu washiriki walio na chini ya umri wa miaka minane tu. 736197