IQNA

Sharja, mwenyeji wa maonyesho ya biashara ya Kiislamu

13:51 - January 26, 2011
Habari ID: 2070499
Idara ya Bishara na Viwanda ya Sharja SCCI imetoa taarifa ikitangaza kuwa itaandaa duru ya 13 ya maonyesho ya kibiashara ya Kiislamu sambamba na duru ya 14 ya kikao cha sekta binafsi ya nchi za Kiislamu nchini humo tokea tarehe 24 hadi 19 Aprili mwaka huu.
Kwa mujibu wa tovuti ya AMEINFO, Ahmad Muhammad al-Madfa' mkuu wa Idara ya Bishara ya Sharja amesema kuwa kuandaliwa kwa pamoja maonyesho na kikao hicho kunawapa washiriki fursa maalumu ya kuarifisha na kushuhudia bidhaa na huduma za kibiashara za nchi za Kiislamu. Amesema kuwa jambo hilo pia linawapa washiriki fursa ya kuchunguza njia za kuondoa vikwazo vinavyozuia kuimarishwa kwa biashara na uwekezaji wa sekta binafsi katika nchi za Kiislamu. Ameongeza kuwa nchi za Kiislamu zina mazingira na uwanja bora wa kuvutia biashara na uwekezaji wa kigeni kutoka pembe zote za dunia.
Al-Madfa' ameongeza kuwa katika hali ya hivi sasa uimarishwaji wa biashara za Kiislamu kote ulimwenguni, bidhaa tofauti, huduma za benki na fedha za Kiislamu na bidhaa za chakula halali una umuhimu mkubwa na kwamba kuandaliwa kwa monyesho na vikao kama hivyo ni hatua muhimu katika kufikiwa lengo hilo. 736412
captcha