Hayo yamesemwa na Mohammad Bagher Khorramshad Mkuu wa Shirika la Mahusiano ya Kiislamu na Utamaduni ICRO.
Khorramshad amesema katika mahojiano na IQNAni kuwa jukumu la vituo vya utamaduni vya Iran kote duniani ni kuarifisha utamaduni wa Qur'ani wa Iran kwa walimwengu. Amesema utamaduni wa Iran una chimbuko katika Qur'ani Tukufu, Uislamu na misingi ya Mapinduzi ya Kiislamu.
“Kuandaa wiki za Qur'ani katika nchi mbalimbali ni moja ya njia za kivitendo za kutekeleza jukumu hili,” amesema mkuu wa ICRO.
Akiashiria mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu yaliyomalizika hivi karibuni hapa nchini, amesema mashindano hayo ni ubunifu mkubwa na kusema yana nukta mbili muhimu nazo ni Qur'ani na wanafunzi wa vyuo vikuu.
736333