Ujumbe huo unaojumuisha wawakilishi wa mashirika ya misaada ya Kiislamu kutoka Ujerumani, Marekani na Misri umetembelea hospitali ya Ash-Shifa katika mji wa Ghaza. Aidha wanaharakati hao wa misaada ya kibinadamu wametembelea Kituo cha Himaya ya Kisaikolojia kinachofungamana na Shirika la Misaada ya Kiislamu Duniani. Aidha wametembelea mayatima, vipofu, watu wenye mahitajio maalumu, familia masikini na familia ambazo nyumba zao zilibomolewa katika hujuma ya kinyama ya utawala wa Kizayuni wa Israel mwaka 2009.
Wananchi wasiopungua milioni moja na nusu wa Palestina wanaishi katika mazingira mabaya na magumu zaidi katika eneo la Ukanda wa Gaza.
Jamii ya Kimataifa imekosoa vikali mzingiro wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza na kusema ni jambo lisilokubalika kwa mzingiro huo kuendelea.
Utawala wa Kizayuni wa Israel unaendeleza jinai zake huko Ghaza kutokana na uungaji mkono unaopata kutoka serikali ya Marekani ambayo hutumia uwezo wake wa kura ya turufu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuzuia hatua kali kuchukuliwa dhidi ya utawala wa Kizayuni.
736741