IQNA

Mashariki ya Kati ya Kiislamu iko njiani inakuja

14:40 - January 29, 2011
Habari ID: 2071369
Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa mjini Tehran amesema kuwa, Mashariki ya Kati ya Kiislamu ambayo itatokana na demokrasia ya Kiislamu ya wananchi iko njiani inakuja.
Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amesema hayo katika hadhara kubwa ya waumini waliohudhuria ibada ya Sala ya Ijumaa katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Tehran na kubainisha kwamba, hivi sasa wananchi wa Mashariki ya Kati wameamka.
Ayatullah Khatami ameashiria matukio ya hivi karibuni nchini Tunisia na vuguvugu la wananchi la kupinga udikteta linaoendelea katika nchi za Misri, Jordan na Yemen na kusisitiza kwamba, matukio haya ni mtikisiko wenye msukumo na mwamko wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran ameashiria kuondolewa madarakani na wananchi Rais wa Tunisia Zainul Abidin bin Ali na kubainisha kwamba, hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowaporomosha maadui wa dini ya Kiislamu.
Kuhusiana na matukio ya Lebanon, Ayatullah Khatami amewataka wananchi wa nchi hiyo kuwa macho na njama za maadui dhidi ya taifa lao.

737541
captcha