IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya wanachuo yafanyike kila mwaka

14:48 - January 29, 2011
Habari ID: 2071427
Imependekezwa kuwa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu yafanyike kila mwaka badala ya kila miaka miwili.
Pendekezo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu wa Iran anayesimamia masuala ya Qur'ani Hujjatul Islam Hamid Muhammadi alipohojiwa na IQNA kuhusu Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu yaliyofanyika katika mji mtakatifu wa Mash'had kaskazini mashariki mwa Iran kuanzia Januari 9-11.
Amesema nukta muhimu katika mashindano hayo ni kuwa wanafunzi vijana kutoka vyuo vikuu mbalimbali duniani wanakutana sehemu moja kushindana na hivyo kutathmini uwezo wao.
Ameongeza kuwa mashindano hayo yanatoa motisha kwa wanachuo kufanya kazi kwa bidii ili kufanikiwa katika mashindano ya baadaye.
Wakati huo huo Hujjatul Islam Muhammad amesema mpango mpya ujulikanao kama: "Kuelekea Maisha ya Qurani" utafanyika pembizoni mwa mashindano yajayo ya Qur'ani ya Kimataifa. Amesema mpango huo utasaidia kuinua kiwango cha maisha ya Kiislamu ya mtu binafsi na jamii katika jamii za Waislamu duniani.
734512
captcha