IQNA

Wazayuni wakosea heshima Qur'ani Tukufu

16:51 - January 29, 2011
Habari ID: 2071946
Katika hatua ya dharau ya moja kwa moja dhidi ya matukufu ya Kiislamu, mkahawa mmoja wa utawala haramu wa Israel unawapa wateja wake vitambaa vya kufutia uchafu ambavyo vimeandikwa juu yake aya za Qur'ani Tukufu.
Vitambaa hivyo ambavyo vimeandikwa aya ya Qur'ani na picha ya Msikiti wa Mtume (saw) wa mjini Madina vinatumiwa kupangusia uchafu mezani katika moja ya mikahawa ya Tel Aviv na kisha kutupwa kwenye maeneo ya taka.
Aya ya 7 ya Surat Muhammad (saw) ambayo inazungumzia jihadi ndiyo iliyoandikwa kwenye vitambaa hivyo vya kufutia uchafu.
Kabla ya hapo pia utawala haramu wa Israel ulichukua hatua kama hiyo ya kukosea heshima matukufu ya Kiislamu kwa kuandika aya za Qur'ani kwenye chupa za plastiki na mikebe ya pombe.
Hivi karibuni utawala huo pia uliandika aya za Qur'ani katika maeneo haramu na ya kuchukiza na vilevile kuteketeza msikiti mmoja huko Nablus huko Palestina. 738016
captcha