IQNA

Taasisi ya kutarjumi Qur'ani ianzishwe

13:42 - January 30, 2011
Habari ID: 2072140
Katika mkutano na Ayatullah Muqtadai Mkuu wa Chuo cha Kidini cha Qum, bodi ya wakurugenzi wa Jumuiya ya Watafiti wa Qur'ani imesisitiza kuhusu umuhimu wa kuanzishwa Taasisi ya Kutarjumi Qur'ani katika Chuo cha Kidini cha Qum.
Mkutano huo uliitishwa kwa lengo la kujadili maandalizi ya kongamano la kuwaenzi watarjumi wa Qur'ani Tukufu.
Hujjatul Islam Muaddab Mkurugenzi wa Jumuiya ya Watafiti wa Qur'ani nchini Iran na Hujjatul Islam Rezai Isfahani, katibu wa kongamano hilo wamewasilisha ripoti ya hatua zilizochukuliwa na kutoa wito wa msaada wa kifedha na kimaanawi kufanikisha kongamano hilo la kimataifa.
Akizungumza katika mkutano huo, Hujjatul Islam Ali Nasiri amesisitiza umuhimu wa kuanzisha taasisi ya kutarjumi Qur'ani chini ya usimamizi wa Chuo cha Kidini cha Qum. Amesema ukosefu wa usimamizi ni jambo linalopelekea kuwepo tarjumi dhaifu za Qur'ani.
Pendekezo la kuasisiwa Taasisi ya Kutarjumi Qur'ani katika Chuo cha Kidini cha Qum imekaribishwa na bodi ya chuo hicho na imeamuliwa kuwa suala hilo lijadiliwe kwa kina katika kongamano la kuwaenzi watarjumi wa Qur'ani.
738116
captcha