Benki Kuu ya Mauritius imetangaza kuwa habari zaidi kuhusu benki ya kwanza ya Kiislamu nchini himo zitatolewa hivi karibuni.
Nchi ya Mauritius imekuwa katika jitihada za kuzidisha thamani za uchumi wa Kiislamu na imepangwa kuwa Benki Kuu ya nchi hiyo itaanza kutoa huduma za kibenki kwa mujibu wa sheria za Kiislamu.
Benki Kuu ya Mauritius ilitoa kibali cha kwanza cha benki ya Kiislamu mwaka 2009 kwa shabaha ya kubuni mbinu mbadala ya huduma za masuala ya kifedha.
Mfumo wa benki wa Kiislamu ambao umekuwa na kiwango cha juu zaidi cha ustawi kati ya mifumo mingine ya kibenki duniani umepewa mazingatio makubwa katika miaka ya hivi karibuni. 738620