IQNA

Mafunzo ya Qur'ani Tukufu kupitai mtandao nchini Qatar

16:57 - January 30, 2011
Habari ID: 2072628
Taasisi ya Dar al-Qur'an ya Qatar inayofungamana na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya nchi hiyo imeanzisha mafunzo ya Qur'ani Tukufu kupitia mtandao katika mji mkuu wa nchi hiyo Doha kwa ushirikiano wa Shirika la Mji wa Eletroniki la nchi za Kiarabu.
Akizungumzia suala hilo Nami bin Yusuf an-Nami, Katibu Mkuu wa shirika hilo amesema kuwa hiyo ni mara ya kwanza kwa zeozi hilo la mafunzo ya Qur'ani kupitia suhula za elektroniki kufanyiwa majaribio nchini Qatar kwa usimamizi wa Dar al-Qur'an.
Amesema mipango ya masomo kupitia mbinu za elektroniki ni mbinu mpya inayotumiwa sana kueneza masomo ya Qur'ani ulimwenguni na kwamba wanaotumia mtandao wa intaneti wana fursa nzuri ya kunufaika kwa njia tofauti na mipango hiyo.
Nami amesema kuwa lengo la kutumiwa mbinu hiyo ya mafunzo ni kueneza kwa haraka na katika sehemu kubwa ya dunia maarifa ya Kiislamu na Qur'ani. 738886
captcha