IQNA

Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu kusherehekewa katika misikiti 32000 Iran

12:55 - January 31, 2011
Habari ID: 2072811
Maadhimisho ya mwaka wa 32 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu yatafanyika katika misikiti 32000 kote nchini Iran.
Hujjatul Islam Hamid Reza Arbab Suleiman ambaye ni mkuu wa masuala ya misikiti katika taasisi ya Utamaduni na Sanaa amesema kuwa hafla maalumu zitafanyika katika misikiti kwa mnasaba wa sherehe za Alfajiri 10.
Akiashiria nafasi muhimu ya misikiti katika jamii za Waislamu Hujjatul Islam Arbab Suleiman amenukulu aya ya 96 ya suratu Al Imran katika Qur'ani Tukufu isemayo: “Hakika Nyumba ya kwanza waliowekewa watu kwa ibada ni ile iliyoko Bakka, iliyo barikiwa na yenye uwongofu kwa walimwengu wote”. Ameongeza kuwa misikiti imekuwa na nafasi muhimu katika Mapinduzi ya Kiislamu.
Hujjatul Islam Hamid Reza Arbab Suleiman ambaye pia ni mshauri wa Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu amesema warsha kuhusu ‘Mapinduzi ya Kiislamu , Msikiti na Uono wa Mbali’ zitafanyika kote Iran kwa mnasaba wa sherehe hizo za kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
738085
captcha