Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA mjini Mash'had, semina hiyo itafanyika kwa lengo la kuhakikisha kuwa vyuo na wanazuoni wa kidini wanatumia zaidi mitandao ya intaneti na maktaba za dijitali.
Kuchunguza nafasi ya mitandao ya intaneti katika kuhubiri dini na kuwafanya wanazuoni wa kidini wapate ujuzi zaidi kuhusu matumizi ya intaneti ni mambo yatakayojadiliwa kwa kina katika semina hiyo.
Aidha pembizoni mwa semina hiyo kutakuwa na vikao maalumu vya kielimu kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu uga wa intaneti. 738062