Kwa mujibu wa tovuti ya kituo hicho, maombolezo hayo yatakayoanza saa 12:30 kwa wakati wa New York yataendelea kwa muda wa masaa matatu.
Usomaji wa sura ya Yasin, dua ya Tawassul na ziara ya Mtume Muhammad (saw) ni miongoni mwa ratiba za maombolezo hayo ambayo yataendeshwa kwa lugha mbili za Kiingereza na Kiurdu. Kituo hicho cha Kiislamu pia kimeandaa maombolezo ya kukumbuka kifo cha mtukufu mwingine wa Kiislamu Imam Ali bin Mussa Ridha (as) ambaye ni mjukuu wa Mtume (saw) katika siku ya Jumatano. 739390