IQNA

Jeshi la Iran kushiriki katika mashindano ya Qur'ani Saudi Arabia

12:50 - February 01, 2011
Habari ID: 2073634
Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran litashiriki katika Mashindano ya Kuhifadhi Qur'ani ya Wanajeshi wa Nchi za Kiislamu yatakayofanyika Saudi Arabia.
Hayo yamedokezwa na Hujjatul Islam Muhammad Ali Al Hashemi Mkuu wa Idara ya Itikadi na Siasa katika Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Ameongeza kuwa majeshi ya Iran tayari yameshafanya mashindano ya pamoja ya Qur'ani na nchi za Kiislamu kama vile Oman, Pakistan na Saudi Arabia.
Aidha amesema awamu ya tatu ya mashindano ya Qur'ani ya majeshi ya Iran na Oman ilimalizika hivi karibuni mjini Tehran.
Hujjatul Islam Muhammad Ali Al Hashemi amesema mashindano ya kimataifa ya Qur'ani baina ya majeshi ya nchi za Kiislamu ni hatua ya kuimarisha amani na urafiki baina ya nchi hizo. Amesema mashindano hayo pia huandaa mazingira ya ushirikiano wa majeshi ya nchi za Kiislamu jambo ambalo linapelekea kuimarika umoja na mshikamano katika umma wa Kiislamu.
739040
captcha