IQNA

Mashindano ya Qur'ani kufanyika Oman

12:54 - February 01, 2011
Habari ID: 2073635
Kituo cha Sultan Qaboos cha Utamaduni wa Kiislamu (SQCIC) kimetangaza kuanza usajili wa mashindano ya 21 ya Kuhifadhi Qur'ani yanayofadhiliwa na Sultan Qaboos.
Kwa mujibu wa gazeti la Oman Tribune, Ali Bin Abdullah Al Saqri Naibu Mkurugenzi wa mashindano ya Kuhifadhi Qur'ani yanayofadhiliwa na Sultan Qaboos amesema wanaotaka kushiriki katika mashindano hayo wanapaswa kujaza fomu maalumu zinazopatikana katika misikiti ya maeneo ya Nizwa, Ibra, Ibri, Adam, Sohar, Rustaq, Diba, Sur na Salalah, na vilevile, msikiti wa Sultan Said Bin Taimour huko Al Khuwair, msikiti wa Sayyid Tariq Bin Taimour huko Al Khoud, Idara ya Awqaf na Masuala ya Kidini huko Duqm na Suwaiq, Kituo cha Sayansi ya Kiislamu huko Buraimi na Jaalan Bani Bu Hassan na pia katika Msikiti wa Sinaw.
Siku ya mwisho ya kuwasilisha fomu ni Machi 30 na mashindano ya mchujo yataanza Aprili 19 na kumalizika Aprili 23.
Mashindano hayo yatakuwa na vitengo vitano ambavyo ni kuhifadhi Qur'ani kamili na tajweed, kuhifadhi juzuu 24, kuhifadhi juzuu 18, kuhifadhi juzuu 12 na kuhifadhi juzuu sita.
739504
captcha