IQNA

Masomo ya wanawake ya hifdhi ya Qur'ani Tukufu yaanza Qatar

12:44 - February 01, 2011
Habari ID: 2073870
Masomo maalumu ya wanawake ya hifdhi ya Qur'ani Tukufu yameanza katika Kituo cha Hifdhi ya Qur'ani cha az-Zahra katika mtaa wa al-Ma'mura mjini Doha.
Kwa mujibu wa gazeti la as-Sharq linalochapishwa Qatar, masomo hayo yatakayoanza leo Jumanne yatafundishwa na Randa Jubbara, mkuu wa kitengo cha tafsiri ya Qur'ani Tukufu cha Kituo cha az-Zahra.
Masomo hayo yatakayoendelea kwa muda wa miezi sita yatajumuisha tafsiri na hifdhi ya Qur'ani nzima, masomo tofauti ya Qur'ani, miongozo na kanuni za lugha ya Kiarabu, kanuni za tajwidi na uboreshwaji usomaji Qur'ani.
Kituo cha Hifdhi ya Qur'ani cha az-Zahra cha nchini Qatar kinashurutisha wanafunzi wa masomo hayo ya hifdhi ya Qur'ani wawe na vyeti vya masomo yasiyo chini ya sekondari. Kituo hicho pia kitatoa vyeti maalumu kwa wanafunzi watakaomaliza kwa mafanikio masomo hayo. 740246
captcha