Kituo cha upashaji habari cha Palestine Info kimeripoti kuwa meya wa Kizayuni wa mji unaokaliwa kwa mabavu wa Haifa amepasisha mpango huo na kupuuza mitazamo ya viongozi wa Msikiti wa Istiqbal
Baada ya kupasishwa mpango huo kamati ya msikiti huo imesema hatua hiyo ni sehemu y mpango wa kupora maeneo na milki za Kiislamu za mji unaokaliwa kwa mabavu za Haifa.
Taarifa ya kamati ya uongozi wa msikiti huo imesema kuwa kuporwa milki za Kiislamu na Kiarabu za Haifa si suala la kidini pekee bali ni kadhia ya kitaifa yenye umuhimu mkubwa na itakuwa na taathira mbaya kwa maisha ya Wapalestina wa mji huo.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa kamati hiyo iko tayari kukabiliana na changamoto inayokabili historia na turathi za Kiislamu za mji wa Haifa.
Vilevile imewataka wananchi wa Palestina kuungana kwa ajili ya kukabiliana na siasa za kutumia mabavu, kughusubu na juhudi za kutaka kufuta utambulisho wa Palestina katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni. 740413