Kwa mujibu wa tovuti ya Arabonline, mashindano hayo yameandaliwa na Idara Kuu ya Wakfu na Masuala ya Zaka ya Libya kwa ushirikiano wa Klabu ya Utamaduni, Michezo na Jamii ya Tripoli.
Duru hiyo ya kumi ya mashindano ya hifdhi ya Qur'ani inawashirikisha washindani wa kike 350 kutoka Tripoli ambao wanashindana katika vitengo tofauti vya mashindano hayo. Idara kuu iliyotajwa pia inatayarisha mashindano kama hayo kwa ajili ya wanaume.
Kamati ya mashindano hayo tayari imeandikisha wawanume 125 ambao wamethibitisha kushiriki katika mashindano hayo. 740322