Hayo yamesemwa na afisa wa Idara ya Qur'ani na Hadithi ya Chuo Kikuu cha al Mustafa al Alamiyyah Hujjatul Islam Hamid Ridha Karimi na kuongeza kuwa mkutano huo utafanyika kwa lengo la kubainisha matokeo ya vikao vitano vya kimataifa vya Qur'ani na Hadithi.
Ameongeza kuwa vikao hivyo vilianza juzi tarehe Mosi Februari nchini Albania sambamba na siku ya kurejea nchini hayati Imam Khomeini baada ya kuishi uhamishoni kwa kipindi cha miaka 15. Sheikh Karimi amesema makala bora za vikao hivyo zitawasilishwa katika mkutano wa kimataifa utakaofanyika baadaye mwaka huu.
Kuhusu vikao hivyo vitano, afisa huyo wa Idara ya Qur'ani na Hadithi ya Chuo Kikuu cha al Mustafa al Alamiyyah amesema vikao hivyo vinafanyika kwa shabaha ya kueneza utamaduni wa dua na maombi katika nchi mbalimbali hususan katika nchi zenye wawakilishi wa chuo cha al Mustafa al Alamiyyah.
Amesema vikao hivyo vinafanyika katika nchi za Albania inayowakilishi bara Ulaya, Indonesia inayowakilishi kusini mashariki mwa Asia, Tanzania inayowakilisha Afrika, Afghanistan inayowakilisha nchi jirani na Syria inayowakilisha nchi za Kiarabu.
Sheikh Karimi amesema kikao cha kwanza kinachofanyika nchini Albania kinajadili maudhui ya "athari za dua na maombi na uhusiano wake na aya za Qur'ani Tukufu. Amesema kikao hicho kitachunguza dua zilizopokelewa katika vitabu vya Waislamu.
Amesema vikao vingine vitafanyika katika nchi zilitajwa hapo baadaye. 740439