Sambamba na siku ya kwanza ya sherehe za Alfajiri Kumi za kuadhimisha Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran na tukio la kurejea nchini hayati Imam Khomeini Mwenyezi Mungu amrehemu baada ya kuishi uhamishoni kwa kipindi cha miaka 15, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema Februari Mosi alizuru kaburi la muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu Imam Khomeini MA na kumsomea al Fatiha.