Kwa mujibu wa Mehdi Qarasheikhlu Mkuu wa Kamati ya Qur'ani ya Makao Makuu ya Sherehe za Alfajiri 10, vikao hivyo vitahudhuriwa na maqari maarufu wa kimataifa katika mikoa yote ya Iran.
Katika mahojiano na Kanali ya Televisheni ya Qur'ani mjini Tehran Qarasheikhlu amesema vikao hivyo vitajumuisha pia tamasha za Qur'ani kwa ajili ya watoto, mabarobaro na familia. Amesema sambamba na hayo kutakuwa na makongamano 50 ya Qur'ani katika kipindi cha siku 10 kote Iran.
Ameendelea kusema kuwa mashindano ya intaneti ya “Qur'ani, Kitabu cha Uono wa Mbali” yanaendelea na kuongeza kuwa wanaotaka ksuhiriki katika mashindano hayo wanaweza kutembelea tovuti ya www.telavat.com
Washindi watatunukiwa zawadi Februari 11 ambayo ni siku ya ushindi mwa Mapinduzi ya Kiislamu.
741392