IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Itqan yafanyika Saudi Arabia

13:34 - February 05, 2011
Habari ID: 2075227
Mashindano ya Qur'ani Tukufu yaliyopewa jina la Itqan yamepangwa kufanyika tarehe 14 hadi 17 Februari huko katika mji wa Kharaj nchini Saudi Arabia.
Mashindano hayo yana lengo la kuwashajiisha vijana kuhifadhi, kusoma na kuzingatia zaidi aya za kitabu hicho kitakatifu cha Waislamu.
Kwa mujibu wa gazeti la al-Iqtiswadiya linalochapishwa nchini humo, mashindano hayo ambayo yamedhaminiwa na Kituo cha Masomo ya Qur'ani Tukufu cha mji wa Kharaj yatahusu hifdhi na tafsiri ya Qur'ani.
Muhammad bin Ahmad al-Khunein ambaye ni mkuu wa kituo hicho amesema kwamba washiriki wa mashindano hayo watachuana katika kuhifadhi juzuu tatu za mwisho za Qur'ani Tukufu na pia kufasiri juzuu Amma ambayo ni ya thelathini ya kitabu hicho.
Amesema wanaume ambao watashiriki katika mashindano hayo watashindana katika Madrasa ya Qur'ani ya Sad bin Maadh na wanawake katika Kituo cha Qur'ani cha al-Fadhila. 741382
captcha