IQNA

Kusamehewa wafungwa waliohifadhi Qur'ani Kuwait

13:32 - February 05, 2011
Habari ID: 2075231
Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Kuwait imetangaza habari ya kuachiliwa huru wafungwa waliohifadhi Qur'ani Tukufu.
Kwa mujibu wa gazeti la Gulf News, uamuzi wa kuachiliwa huru wafungwa hao ni sehemu ya juhudi za kuwawezesha kufahamu thamani kubwa za kitabu hicho kitakatifu na hatimaye kuwafanya wawe watu wema katika jamii.
Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa Kuwait amesema kuhusu jambo hilo kuwa hotuba za kidini na mawaidha ni sehemu ya sera na ratiba za wizara hiyo kwa lengo la kuhuisha thamani za kiroho za wafungwa. Amesema ratiba hiyo imewawezesha wafungwa kubadili tabia na mienendo yao mibaya.
Waziri wa Wakfu wa Kuwait amesema wale wanaofanikiwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu watakuwa wakipewa msamaha na kufutiliwa mbali vifungo vyao. Amesema wizara hiyo pia inachunguza pendekezo la kuachiliwa huru katika siku zijazo wafungwa ambao wanasoma vyema Qur'ani. 741415
captcha