Taasisi hiyo imetangaza kuwa masomo hayo pamoja na mbinu za wasomaji mashuhuri wa Qur'ani wa Iraq yataanza kufundishwa hivi karibuni katika mji huo.
Sayyid Hussein Ismail as-Swadr ambaye ni muasisi wa tasisi hiyo ya Qur'ani amesema kuwa masomo hayo yataendeshwa na wasomaji mashuhuri wa Qur'ani akiwemo Sheikh Mahmoud al-Karkhi.
Taarifa ya taasisi hiyo imesema kuwa watu watakaohitimu masomo hayo watapewa vyeti na vibali vya kusoma Qur'ani nchini Iraq na kwingineko. 742489