IQNA

Sherehe za Maulidi ya Mtume kufanyika London

1:27 - February 07, 2011
Habari ID: 2076445
Sherehe za kuadhimisha Maulidi na siku ya kuzaliwa Mtume Muhammad (saw) zitafanyika mjini London Uingereza tarehe 22 Februari.
Tuvuti ya Kituo cha Kiislamu cha London imeripoti kuwa sherehe hiyo ya Maulidi ya Mtume (saw) itafanyika sambamba na ile ya kuzaliwa mjukuu wake Imam Ja’far Swadiq (sa).
Sherehe hiyo itakayohudhiwa na Waislamu hususan wafuasi wa Ahlulbait (as) itakuwa na ratiba mbalimbali zinazotayarishwa na Kituo cha Kiislamu cha London.
Kituo hicho pia kitakuwa na kongamano la Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kwa mnasaba wa kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu Jumamosi ijayo.
Miongoni mwa maudhui zitakazojadiliwa katika kongamano hilo ni pamoja na Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na kueneza uhuru na ya thamani za kiroho, ulinganisho baina ya Mapinduzi ya Kiislamu na mapinduzi mengine mashuhuri duniani, nafasi ya ulimwengu wa Kiislamu katika medani za kimataifa, ujumbe wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na utawala wa thamani za Mwenyezi Mungu, na haki ya wananchi ya kuainisha mambo yao dhidi ya madikteta. 742495
captcha