Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa Morocco Ahmad Taufiq ameashiria nafasi ya mashindano hayo katika nchi mbalimbali duniani na kusema kuwa lengo lake ni kunyanyua ju kiwango cha shughuli zinazohusiana na masuala ya Qur’ani.
Jopo la majaji wa mashindano hayo ambalo limeainishwa na Wizara ya Wakfu ya Moroco linaundwa na wanachama 10 ambao 6 miongoni mwao ni Wamorocco na wanne wanatoka nchi za Saudi Arabia, Libya, Misri na Jordan.
Mashindano hayo yanahusisha sekta za kuhifadhi Qur’ani kamili, tartili na tafsiri na vilevile kuhifadhi hizbu tano, tartili na kiraa ya Qur’ani. 742630