IQNA

Masomo ya Qur'ani kwa wanawake wa Kishia nchini Saudia

14:07 - February 07, 2011
Habari ID: 2076751
Taasisi ya Qur'ani ya Dauhatul Qur'ani ya mji wa Saihat nchini Saudi Arabia imetangaza habari ya kuanzishwa hivi karibuni mafundisho ya Qur'ani kwa wanawake wa Kishia nchini humo.
Masomo hayo ambayo yatachukua miaka minne kukamilika yatahusu utafakari wa aya za Qur'ani, taaluma za Qur'ani, itikadi, fiqhi, balagha, nahau, mbinu za wafasiri, kiraa na tajwidi ya Qur'ani. Usajili wa majina ya walio na hamu ya kushiriki katika masomo hayo ulimalizika siku ya Ijumaa iliyopita na yamepangwa kuanza hivi karibuni.
Watakaohitimu masomo hayo watakuwa na uwezo wa kijishughulisha na masuala mbalimbali ya kijamii na kiutamaduni kwa ajili ya kuandaa vikao na mikutano mbalimbali ya wanawake inayohusiana na Qur'ani Tukufu. Wanaweza pia kujishughulisha na masuala ya uhubiri kama vile utoaji hutuba au uandishi wa vitabu na majarida ya umma yasiyo ya kitaalamu kuhusiana na Qur'ani.
Tasisi hiyo ya Qur'ani iliyoanzishwa mwaka 1424 Hijiria inajishughulisha na malezi ya watu walio na hamu ya kusoma masomo ya Qur'ani Tukufu na kuimarisha mwamko wa Qur'ani katika jamii. 742769
captcha