IQNA

Kituo cha Qur'ani cha Taj al-Wiqar chafunguliwa nchini Qatar

14:01 - February 07, 2011
Habari ID: 2076753
Taasisi ya Masuala ya Kheri na Masomo ya Qur'ani cha Qatar imefungua kituo kipya cha masomo hayo kwa jina la Taj al-Wiqar katika eneo la Abu Mahur mjini Doha ikiwa ni katika juhudi zake za kueneza vituo vya hifdhi ya Qura'ni nchini humo.
Kwa mujibu wa gazeti la as-Sharq linalochapishwa nchini Qatar kituo hicho kipya kimeanzishwa kwa madhumuni ya kuzidisha idadi ya wanafunzi walio na hamu ya kujifunza masomo ya Qur'ani na kuwashajiisha wanawake zaidi washiriki katika masomo hayo.
Kituo hicho ambacho kina suhula za kisasa za mafunzo kinatazamiwa kuimarisha zaidi shughuli za mafunzo ya Qur'ani nchini Qatar.
Vipindi zaidi vya masomo vimeongezwa katika ratiba ya masomo ili kuimarisha viwango vya masomo katika kituo hicho kipya. 742964
captcha