IQNA

Waliozuia wasomaji Qur'ani Nigeria wasailiwa

17:22 - February 07, 2011
Habari ID: 2077060
Gavana wa jimbo la Bauchi nchini Nigeria amewasaili wakuu wa mabaraza ya miji minne ya jimbo hilo baada ya wawakilishi wao kushindwa kushiriki katika mashindano ya 25 ya Qur'ani jimboni humo.
Gavana wa Bauchi Isa Yuguda amewataka wakuu wa mabaraza ya miji minne ya jimbo hilo kutoa maelezo ni kwa nini wakilishi wao hawakushiriki katika mashindano ya kusoma Qur'ani ya jimbo hilo.
Amesisitiza kuwa wakuu wa miji hiyo wanapaswa kutoa maelezo ni kwa nini wamewazuia vijana kushiriki katika mashindano hayo.
Gavana Isa Yuguda amezitaka pia familia za Kiislamu za Nigeria kuwatayarishia uwanja nzuri watoto wao kwa ajili ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu.
Mashindano ya 25 ya kusoma Qur'ani ya jimbo la Bauchi yalifanyika tarehe 30 Januari yakiwashirikisha wasomaji 140. 743443


captcha