IQNA

Mashindano ya kimataifa ya wanajeshi ya Qur'ani Tukufu kufanyika Saudi Arabia

14:22 - February 08, 2011
Habari ID: 2077592
Duru ya sita ya mashindano ya hifdhi ya Qur'ani Tukufu kwa wanajeshi ipepangwa kufanyika hivi karibuni nchini Saudi Arabia katika mji mtakatifu wa Makka.
Akizungumzia suala hilo Abdallah bin Swalih Aal al-Sheikh, msimamizi mkuu wa mashindano ya kimataifa ya hifdhi ya Qur'ani Tukufu kwa wanajeshi wa Saudi Arabia amesema kuwa wanajeshi kutoka nchi tofauti za Kiarabu na Kiislamu watashiriki katika mashindano hayo. Amesema ratiba nyingine zitakazotekelezwa kwenye mashindano hayo ni pamoja na hotuba za kimaanawi za wanazuoni na wanafikra wa Kiislamu na vilevile masomo na mbinu za hifdhi ya Qur'ani Tukufu.
Al-Sheikh amesema kuwa mashindano hayo yatafanyika katika hatua nne za hifdhi ya Qur'ani nzima pamoja na tartili na tajwidi, hifdhi ya juzuu 20 pamoja na tartili na tajwidi, hifdhi ya juzuu 10 pamoja na tartili na tajwidi na hifdhi ya juzuu tano pamoja na tartill kwa kuchunga sheria za tajwidi.
Kamati inayosimamia mashindano hayo imetangaza kwamba sharti kuu la kushiriki kwenye mashindano hayo ni kwa washiriki kuwa wanajeshi na kuhudumu kwenye jeshi kwa kipindi kisichopungua miaka miwili.
Sharti jingine ni kuwa watu walioshiriki kwenye mashindano hayo mwaka uliopita na kushinda nafasi muhimu hawaruhusiwi kushiriki tena kwenye vitengo walivyoshiriki mwaka huo bali wanapasa kushiriki kwenye vitengo tofauti tena vya juu.744040
captcha