Tovuti ya Shiite News imeripoti kuwa uamuzi wa kuanzisha mpango huo ulichukuliwa jana katika mkutano wa kwanza wa Taasisi ya Kuwainga Mkono Wapalestina.
Washiriki katika mkutano huo wameitaka Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) na Umoja wa Ulaya kutafuta njia za kutatua kadhia ya Palestina na kuzuia unyama na ukatili unaofanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya wananchi wasiokuwa na ulinzi wa Palestina.
Mkutano huo pia umebuni mipango ya mwaka mzima ya kuwaunga mkono wananchi wa Palestina.
Vilevile washiriki wamekubaliana kuhuisha haki za wananchi wa Palestina, kukomboa msikiti wa al Aqsa na kupambana na utawala wa Kizayuni. 744172
.