Tovuti ya Gulf Times imeripoti kuwa semina hiyo imefanyika kwa himaya ya kundi la Sasco na kuhudhuriwa na watu zaidi ya 100.
Semina hiyo imehutubiwa na Mkurugenzi wa Benki ya Kiislamu ya QNB Musaddiq al Malik ambaye amefafanua misingi ya mfumo wa benki wa Kiislamu kwa mujibu wa sheria za dini hiyo na mafanikio yake.
Semina hiyo pia imejadili mabadiliko yaliyosababishwa na mfumo wa benki wa Kiislamu katika benki za kawaida na viwango vya uhasibu vinavyotumiwa na Jumuiya ya Uhasibu na mahesabu ya Taasisi ya Fedha ya Kiislamu (AAOIFI). 744083