Akihutubia sherehe hiyo, Roters amesema anayejenga hubakia milele na kwamba ujenzi wa msikiti huo ni kuimarisha uhusiano baina ya Waislamu na nchi zao. Amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo umekabiliwa na matatizo mengi na kwamba mambo mengi ya kiufundi na matakwa ya wakazi wa eneo hilo yalipaswa kuzingatiwa.
Meya wa Cologne pia ameushukuru Umoja wa Kiislamu wa Kituruki (Türkisch-Islamische Union) ambao ndio uliotekeleza mradi huo kwa kufanya juhudi kubwa za kuanzisha uhusiano na kujenga mawasiliano ya kuwepo mazungumzo.
Imam wa jamaa wa msikiti huo Saban Kondi pia amesema kuwa msikiti wa Cologne ni nembo ya usawa, amani na urafiki na kuongeza kuwa watu wote wanaruhusiwa kuutembelea. 744051