IQNA

Sauti bora ya Qur'ani kuchaguliwa Tulkaram Palestina

10:58 - February 09, 2011
Habari ID: 2078210
Mkuu wa Idara ya Wakfu ya mji wa Tulkaram nchini Palestina ametangaza kuanza usajili wa majina ya washiriki wa mashindano ya Qur'ani kwa lengo la kuchagua sauti bora na ya kuvutia zaidi ya usomaji Qur'ani katika mji huo.
Akizungumzia suala hilo Ad'nan Said, Mkuu wa Idara ya Wakfu ya Tulkaram amesema kuwa mashindano hayo yatakayowashirikisha washindani walio na umri wa chini ya miaka 20 yatafanyika kwa ushirikiano wa televisheni ya al-Fajr al-Jadid ya mji huo. Amesema mashindano hayo yatafanyika katika makundi mawili ya wavulana na wasichana na kwamba tarehe ya kufanyika kwake itajulikana mara baada ya kumalizika shughuli ya usajili wa majina.
Ad'nan Said amesema mara tu baada ya kukamilika mashindano hayo sherehe ya kuyafunga na kuwaenzi washindi itafanyika na kutangazwa moja kwa moja kupitia televisheni ya al-Fajr al-Jadid. 744925
captcha