Olivier Bitz, naibu meya wa mji huo ameshiriki katika sherehe ya ufunguzi wa kituo hicho.
Kwa mujibu wa tovuti ya OUMMA Bits Olivier Bitz amewaambia Waislamu wa eneo hilo kwamba ofisi ya meya wa mji huo imejaribu kukidhi mahitaji yote ya Waislamu wakazi wa mji huo kwa kuwafungulia tena msikiti mkuu pamoja na kuwajengea makaburi maalumu.
Akizungumza katika sherehe hiyo, Aziz al-Alwani mkuu wa kituo hicho amewapongeza viongozi wa ofisi iliyotajwa kwa ushirikiano wao mzuri katika ujenzi wa kituo hicho ambacho ujenzi wake ulikuwa umesimamishwa kutokana na msimamo mbaya wa viongozi wa zamani wa ofisi hiyo. , Waislamu wa Strasbourg wamekuwa wakiishi kwa amani na maelewano na wafuasi wa dini na tamaduni tofauti katika mji huo licha ya kuenea chuki dhidi ya Uislamu na ubaguzi nchini Ufaransa. 745362