Kongamano hilo limefanyika kwa hima ya viongozi wa Kituo cha Kiislamu cha Uingereza.
Kongamano hilo limefanyika baada ya swala ya Magharibi na kuhudhuriwa na maulamaa na wanafikra na kujadili mabadiliko yaliyotokea katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Wanafikra na wanazuoni hao wametoa hotuba mbalimbali wakizungumzia nafasi ya ulimwengu wa Kiislamu katika medani za kimataifa, ujumbe wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, mlinganisho baina ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na mapinduzi mengine duniani na haki ya wananchi ya kujiamulia mambo yao mkabala wa tawala za kidkteta. 746041