IQNA

Maafisa wa Copenhagen waafiki ujenzi wa Msikiti wa Ijumaa

16:23 - February 14, 2011
Habari ID: 2080871
Maafisa wa mji wa Copenhagen, mjii mkuu wa Denmark baada ya muda mrefu wa kusitasita hatimaye wamekubali ombi la Waislamu la kujengwa Msikiti wa Ijumaa katika mji huo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press, kufuatia kukubaliwa ombi hilo Baraza la Waislamu wa Denmark limetangaza kuwa litaanzisha juhudi za kukusanya fedha za kujengwa msikiti wa kwanza katika mji huo.
Licha ya kuwepo upinzani mkali wa chama kinachopinga wajahiri nchini Denmark, lakini Baraza la Mji wa Copenhagen hivi karibuni limepasisha mpango wa kujengwa msikiti huo mkuu wa Waislamu. Baraza la Waislamu wa Denmark limetangaza kuwa ujenzi wa msikiti huo utagharimu karibu dola milioni 37 za Marekani.
Wahajiri wa Kiislamu wa Denmark wamekuwa wakipigania ujenzi wa msikiti huo tokea muongo wa 70 lakini mpango wa kujengwa kwake umekuwa ukipingwa na watawala wa Denmark.
Waislamu wanaunda asilimia 4 ya watu milioni 5.5 wa nchi hiyo. 747197
captcha