IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Iran

17:09 - February 14, 2011
Habari ID: 2080911
Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yameanza Februari 14 mjini Tehran.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yana washiriki 654.
Mashindano hayo yana vitengo kumi vikiwemo, qiraa, hifdhi, utafiti, tarteel. Ufahamu wa maana ya aya za Qur'ani na adhan.
Ili kuinua kiwango cha washiriki, pembizoni mwa mashindano hayo kutakuwa na kozi za kielimu.
Akihutubia katika sherehe za ufunguzi wa mashindano hayo Generali Asudi Mkuu wa Masuala ya Utamaduni na Ulinganiaji katika Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema Qur'ani Tukufu ni bahari isiyo na kikomo ya miujiza isiyo na kifani ya Mwenyezi Mungu.
Mashindano hayo yanatazamiwa kumalizika Februari 16.
746333
captcha