IQNA

Rais Museveni wa Uganda awataka Waislamu wa nchi hiyo kuungana

17:05 - February 14, 2011
Habari ID: 2080916
Rais Yoweri Museveni wa Uganda Jumapili ya jana alikutana na maulamaa wa Kiislamu na kusisitiza juu ya udharura wa Waislamu wa nchi hiyo kuungana.
Kituo cha habari cha Uganda Media Center kimeripoti kuwa Rais Yoweri Museveni amewataka maulamaa wa Kiislamu wa Uganda kushirikiana na kuimarisha umoja wao. Amesisitiza kuwa umoja na mshikamano ni jambo la dharura kwa ajili ya amani na utulivu wa Uganda.
Kumekuwapo mivutano ya muda mrefu sasa kati ya makundi mawili ya Waislamu nchini Uganda, suala ambalo linatishia umoja wa wafuasi wa dini hiyo. 747727
captcha