Hujjatul Islam Yusuf Muqaddam ambaye ni mkuu wa taasisi hiyo amesema juzuu ya nane tayari imeshachapishwa na kwamba juzuu ya tisa itachapishwa hivi karibuni. Amesema insaiklopidia hiyo itachapishwa na Shirika la Bostan-e-Kitab la Qum.
Ameongeza kuwa insaiklopidia hiyo itakuwa na makala kuhusu Qur'ani na vilevile maelezo kuhusu ibara na ufahamu wa Qur'ani, historia ya tafsiri za maudhui muhimu katika Qur'ani Tukufu.
Kuhusu mbinu mbalimbali za kufasiri Qur'ani, Hujjatul Islam Yusuf Muqaddam amesisitiza kuwa juhudi zimefanyika na kuhakikisha mbinu mbalimbali za kufasiri kama vile kutegemea hadithi za Mtume SAW, Ahlul Bayt AS, Masahaba na Ijtihad zinazingatiwa.
Amesema mipango inafanyika ya kuchapisha juzuu za 10 na 11 za Insaiklopidia ya Qur'ani Tukufu.
746867