Duru ya 11 ya masomo ya Qur'ani Tukufu kwa vijana wadogo walio na umri wa zaidi ya miaka 10 itaanza Jumapili ya tarehe 20 Februari katika mji wa Khuweilidiya katika mkoa wa Qatif, mashariki mwa Saudi Arabia.
Masomo hayo ambayo yatachukua muda wa wiki sita yametayarishwa na Kamati ya Masomo ya Qur'ani ya Mimbar al-Hidaya ya mji wa Khuweilidiya.
Kamati hiyo imetangaza kwamba vijana walio na hamu ya kushiriki kwenye mashindano hayo wanaweza kufika kwenye ofisi za kamati hiyo katika mji uliotajwa kwa madhumuni ya kujiandikisha. Muda wa mwisho wa uandikishaji huo ni hapo kesho Jumatano tarehe 15 Februari. 747664