IQNA

Wazayuni wapanua ujenzi wa vitongoji vya Wazayuni Palestina

17:17 - February 15, 2011
Habari ID: 2081550
Utawala wa Kizayuni wa Israel umepasisha mpango wa kujenga makanisa 19 na nyumba 124 za walowezi wa Kiyahudi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Quds Tukufu huko Palestina.
Shirika la habari la Kuwait (KUNA) limeripoti kuwa kwa mujibu wa mpango huo, utawala haramu wa Israel utajenga nyumba 124 za walowezi wa Kiyahudi kaskazini mwa mji wa Quds na makanisa 19 karibu na mlima Abu Ghunaim.
Israel imejenga mamia ya nyumba za walowezi wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Quds Tukufu katika miezi michache ya hivi karibuni licha ya upinzani mkali wa jamii ya kimataifa. 748096

captcha