Sherehe za ufunguzi wa mashindano hayo zilihudhuriwa na Saud bin Swaqr al-Qasimi mtawala wa Ra'sul Kheimah na Swalah al-Budeir, hatibu na imam wa Msikiti wa Mtume (saw) ambaye alikuwa mgeni wa heshima katika sherehe hizo.
Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na washindani 176 wanaoshiriki katika mashindano hayo.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka kwenye mashindano hayo wanawake wanaoshiriki katika vitengo mbalimbali vya kuhifadhi Qur'ani nzima, juzuu, 20, 10 na juzuu tano za kitabu hicho kitakatifu wataruhusiwa kuonyesha vipawa vyao katika hifdhi hizo hadi siku ya Ijumaa.
Wanaume wanaoshiriki katika vitengo vilivyotajwa pia watashindana hadi siku ya Jumamosi tarehe 19 Februari.
Sherehe za kufanga mashindano hayo zitafanyika tarehe 24 ambapo Saud bin Saqr al-Qassimi atahudhuria.
Wahubiri na wanazuoni wa Kiislamu watatoa hotuba na mawaidha mbalimbali ya kidini pambizoni mwa mashindano hayo. 748851